23 Mar 2023 / 115 views
Sevilla waachana na kocha wao

Klabu ya Sevilla imemfukuza wao Jorge Sampaoli kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo ambapo wapo nafasi ya pili kutoka chini kwenye eneo la kushuka daraja.

Kocha huyo wa zamani wa Chile na Argentina, 63, alijiunga na Sevilla mwezi Oktoba kwa mara ya pili kama kocha.

Wamepoteza mechi tano kati ya saba zilizopita na kwa sasa wako nafasi ya 14 kwenye jedwali. Hata hivyo, wametinga robo fainali ya Ligi ya Europa na watamenyana na Manchester United katika mechi mbili za mkondo mwezi ujao.

Mechi ya mwisho ya Sampaoli kuongoza ilikuwa kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wapambanaji wenzake Getafe na kuwafanya wabaki na pointi 28 wakiwa wamesalia na michezo 12.

Sevilla walisema "tayari wanafanya kazi ya kuajiri kocha mpya haraka iwezekanavyo". Mechi yao ya kwanza baada ya mapumziko ya kimataifa ni Cadiz iliyo nafasi ya 15 Jumamosi, Aprili 1.